SERIKALI YAIMARISHA TEHAMA MAHAKAMANI

 

SERIKALI YAIMARISHA TEHAMA MAHAKAMANI

SERIKALI YAIMARISHA TEHAMA MAHAKAMANI

TANZANIA
Serikali  ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji haki kwa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya usikilizaji wa mashauri, utunzaji wa kumbukumbu, ukusanyaji wa takwimu na utoaji wa taarifa za kimahakama unaofahamika kama JUDICIAL STATISTICAL DASHBORD SYSTEM pamoja na matumizi ya Video Conference katika kuendesha mashauri ya usuluhishi ya kimataifa na hata baadhi ya mashauri ya ndani. 
Aidha, Mahakama imeanza majaribio ya matumizi ya teknolojia ya akili mnemba ya kunakili na kutafsiri lugha ya mawasiliano wakati wa mwenendo wa usikilizwaji wa mashauri mahakamani.
Mifumo hii imewezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake na kuendesha mashauri na utoaji haki kwa haraka.