RAIS DKT SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS WA SOMALIA MHE. MOHAMUD
DAR ES SALAAM
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud leo januari 29, 2025 kwenye makazi yake Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Katika hatua nyingine Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini Mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana na katika masuala ya Ulinzi ma Usalama na kubadilishana Wafungwa.
Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025, Jijini Dar es Salaam, upande wa Tanzania imewakilishwa na wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi na Somalia imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi.
Mkataba huo utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa ili waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa