RAIS DKT SAMIA AMPONGEZA ASKOFU MTEULE ROMANUS
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kwa kuteuliwa na papa Francisko kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Iringa.
Kupitia Mitandao ya Kijamii Mhe Rais Samia ameandika
"Pongezi za dhati kwa Baba Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kwa kuteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Iringa. Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa ya Kanisa kwa utumishi wako. Nakutakia kila la kheri.
Mwenyezi Mungu akushike mkono, akubariki na kukuongoza, unapoendelea kushiriki kazi yake ya kuijenga jamii yetu kuwa bora zaidi katika jukumu hili jipya.
Kutoka: 4:12
“Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.”