DKT SAMIA ATOA POLE, KIFO CHA SHEIKH MUHAMMAD IDDI (ABUU IDDI)

 

DKT SAMIA ATOA POLE, KIFO CHA SHEIKH MUHAMMAD IDDI (ABUU IDDI)

DKT SAMIA ATOA POLE, KIFO CHA SHEIKH MUHAMMAD IDDI (ABUU IDDI)

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia, Mufti Mkuu wa Tanzania, Waislamu wote nchini, ndugu, jamaa, marafiki kufuatia kifo cha cha Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi) kilichotokea leo Alhamisi Januari 30, 2025.
Dkt samia kupitia mitandao ya kijamii ameandika ”Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi), Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mwinyiamani, Mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana na Mratibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, kilichotokea leo Alhamisi, Januari 30, 2025.
Natoa salamu za pole kwa familia, Mufti Mkuu wa Tanzania, Waislamu wote nchini, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu. Tumeondokewa na mtu aliyeipenda nchi yake, mwalimu katika imani, mlezi wa wengi katika imani, mpenda haki, mpenda ukweli, umoja, amani na utulivu wa nchi yetu, aliyetumia muda wake mwingi kuyasimamia na kufundisha hayo kupitia mawaidha yake. Mwenyezi Mungu ampe Kauli Thabit, amsamehe makosa yake, amzidishie katika mizani mema aliyotenda, na ampe nafasi katika Pepo yake. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.Ameandika Rais Dkt Samia.