2024 TIC YASAJILI MIRADI 842

 

2024 TIC YASAJILI MIRADI  842

2024 TIC YASAJILI MIRADI  842

TANZANIA
Serikali kupitia Kituo cha uwekezaji  (TIC) mwaka 2024 kimesajili jumla ya miradi mipya 842  yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 7.7 (zaidi ya shilingi  trilioni 18/-) na inatarajiwa kubuni zaidi ya nafasi za kazi 204,000 na kufikia asilimia 84.2 ya lengo kuu la 1,000, ikilinganishwa na miradi 526 iliyosajiliwa mnamo 2023.
Kati ya miradi iliyosajiliwa, 768 ni mpya, huku iliyosalia ikiwa ni miradi ya upanuzi  na Kwa upande wa umiliki, 290 ni uwekezaji wa ndani, 367 ni uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDIs), na iliyosalia ikiwa ni ya ubia.
Ongezeko hili linawakilisha ongezeko kubwa la ukuaji wa uchumi wa nchi na kudhihirisha shauku kubwa kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika soko linaloibukia la Tanzania.
Aidha Mwaka 2021, Tanzania ilisajili miradi yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.7 (kama trilioni 9/-), wakati mwaka 2023, miradi 526 yenye thamani ya takriban shilingi trilioni 14 ilisajiliwa, ikilinganishwa na miradi 293 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10 mwaka 2022.
KUMBUKA:- Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alisaini Sheria mpya ya Uwekezaji ya 2022  ambayo inatoa motisha ya kifedha kwa miradi ya upanuzi na ukarabati, kuruhusu wawekezaji kufurahia misamaha ya ushuru wa bidhaa za mtaji kama vile mashine na mitambo.
Sheria pia ilipunguza kiwango cha mtaji kwa wawekezaji wa ndani kutoka dola 100,000 za Marekani (242m/-) hadi dola 50,000 za Marekani (121m/-).