TSH BIL 600 KUJENGA MELI YA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

 

TSH BIL 600  KUJENGA MELI YA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

TSH BIL 600  KUJENGA MELI YA MIZIGO ZIWA TANGANYIKA

KIGOMA
SERIKALI imeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa meli ya mizigo yenye uzito wa tani 3,500 katika Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya biashara na usafiri wa kikanda.
Kandarasi ya mradi huo tayari imesainiwa na kazi inatarajiwa kuanza hivi karibuni. 
Aidha, meli za MV Liemba, MV Mwongozo na MT Sangara (ambazo hubeba mafuta ya petroli) zinazofanya kazi katika Ziwa Tanganyika hivi sasa zinaendelea kufanyiwa matengenezo Katika Mkoa huo.
ZINGATIA:- Uwekezaji wa serikali katika kukarabati meli hizo tatu unachangiwa na uimara wake, hivyo kusaidia kuokoa gharama ikilinganishwa na kujenga meli mpya.