MIRADI 74 YA PPP KUTEKELEZWA

 

MIRADI 74 YA PPP KUTEKELEZWA

MIRADI 74 YA PPP KUTEKELEZWA

ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali kwa mwaka 2024,  katika kuendelea kushirikiana na sekta binafsi na kuhamasisha uwekezaji kwa njia ya ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public-Private-Partnership - PPP)  imefanikisha upatikanaji wa jumla ya miradi 74 ya PPP ambayo ipo katika hatua mbalimbali za maandalizi na utekelezaji.
 “Katika kufanikisha hilo mpaka sasa kuna jumla ya miradi 74 ya Ubia ambayo ipo katika hatua mbalimbali za maandalizi na utekelezaji, Hadi kufikia mwezi Desemba 2024, miradi 4 imefikia hatua ya utekelezaji, ambapo miradi miwili 2 ni ya uendeshaji wa bandari inayosimamiwa na TPA”Amesema Dkt Samia.
Dkt Smia ameongeza  kuwa iliyotokana na PPP ni Ujenzi wa Jengo la Biashara (Business Complex) kubwa kuliko zote Kariakoo na wa Ubungo - East African Logistic.  Huku Miradi mingine inayotazamiwa kuanza utekelezaji mwaka huu 2025 ni ujenzi wa barabara ya Haraka (Express way) kutoka Kibaha- Chalinze - km 78.9, mradi wa Ukaguzi wa lazima wa vyombo vya moto chini ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) chini ya DART na mradi wa Ujenzi wa Jengo la Biashara na Hoteli ya Nyota Nne katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Kwaheri na Asante 2024, Karibu 2025