KV 400 KUIMARISHA ZAIDI UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI
DODOMA
Tanzania imeandika historia nyingine ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme, hii ni baada ya kuzindua njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma na vituo vya kupoza umeme kilovoti 400 kutoka Chalinze –Pwani na Zuzu-Dodoma.
Mradi huo wa umeme umezinduliwa Desemba 11, 2024 na utawezesha umeme wote unaozalishwa katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP kufika katika maeneo ya kanda ya kaskazini,kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini,kati na Magharibi,kwenye migodi na viwanda, lengo likiwa ni kuimarisha biashara ya umeme Mashariki na Kusini mwa Afrika.
