DKT SAMIA NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE USHAWISHI DUNIANI –FORBES
USA
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi duniani , hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye jarida maarufu ulimwenguni la Forbes.
Hii ni mara ya tatu mfululizo jarida hilo limemtangaza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani.
Forbes wamemtaja Rais Samia kwenye nafasi ya 91 kutoka 95 aliyotajwa kwenye orodha ya mwaka 2023 ambapo amepanda kwa nafasi nne zaidi.
Mbali na hayo, Dkt. Samia anakuwa mwanamke pekee kwenye orodha hiyo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na miongoni mwa wanawake wanne pekee wanaowakilisha Afrika.
