SERIKALI KUONGEZA NGUVU SEKTA YA ELIMU
TANZANIA
Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua kuboresha utoaji elimu katika maeneo ya jumla na ya amali ili kuwezesha kudhibiti ubora wa shule na kubuni mbinu mbalimbali zitakazowezesha wanafunzi kuwa na ujuzi ikiwemo fursa za kujiajiri pasipo subiri kuajiriwa.
Hadi hivi Mikakati mbalimbali imewekwa na serikali katika kuhakikisha wanatumia mbinu za kuhamasisha washiriki kwenye ushiriki wa jamii ikiwemo kupeleka maendeleo shuleni , kufanya ufuatiliaji na tathimini ya udhibiti ubora wa shule wa ndani.
Aidha mafunzo ya amali yatasaidia wanafunzi kupata fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwemo kufikia Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 pamoja na ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.
