RAIS DKT SAMIA AMPONGEZA JOHN MAHAMA KUCHAGULIWA RAIS WA GHANA

 

RAIS  DKT SAMIA AMPONGEZA JOHN MAHAMA KUCHAGULIWA RAIS WA GHANA

RAIS  DKT SAMIA AMPONGEZA JOHN MAHAMA KUCHAGULIWA RAIS WA GHANA

ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mhe John Dramani Mahama kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Ghana  kufuatia uchaguzi uliofanyika  Desemba 2024.
Salamu hizo za pongezi Mhe Rais Samia amezitoa kupitia mitandao ya Kijamii ambapo ameandika,
"On behalf of the Government and the people of the United Republic  of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency, John Dramani Mahama, President-elect of the Republic of Ghana, on being entrusted by the Ghanaian people to lead them as their President. 
I am looking forward to working together, to strengthen our bilateral relations for the benefit of the people of Tanzania and Ghana"
“(Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa John Dramani Mahama, Rais Mteule wa Jamhuri ya Ghana kwa kukabidhiwa na wananchi wa Ghana kuwaongoza kama Rais wao 
Natarajia kufanya kazi kwa pamoja, kuimarisha uhusiano wetu baina ya nchi kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Ghana)”