“LINDENI MAJIMBO, LAKINI FANYENI KAZI” DKT SAMIA
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule( walioteuliwa kutokana na nafasi za ubunge) kufanya kazi kwa bidii huku wakiendelea kuyalinda majimbo yao.
Mhe Rais Samia ametoa wito huo leo Desemba 10, 2024 Ikulu Ya Tunguu visiwani Zanzibar wakati akiwaapisha viongozi aliowateua Desemba 8, 2024.
Dkt Samia amesema “nataka mkafanye kazi vizuri, nataka mkashirikiane na mtakaowakuta, lindeni majimbo lakini mkafanye kazi pia”
Bimkubwa Tanzania tunawatakia majukumu mema, nendeni mkatangulize maslahi ya Taifa mbele.
