TSH MIL 220 ZABORESHA MIUNDOMBINU YA UTALII TABORA ZOO

 

TSH MIL 220 ZABORESHA MIUNDOMBINU YA UTALII TABORA ZOO

TSH MIL 220 ZABORESHA MIUNDOMBINU YA UTALII TABORA ZOO

TABORA
Zaidi ya shilingi Millioni 220 zimetolewa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya utalii ndani ya bustani ya wanyamapori hai "Tabora ZOO".
Miundombinu iliyoboreshwa ndani ya bustani hiyo ni jengo la wananchi kupata taarifa za vivutio vya utalii vinavyopatikana katika bustani hiyo na Kanda ya Magharibi Kwa ujumla (Visitors Information Centre - VIC), vyoo vya kisasa Kwa ajili ya wageni na mabanda ya wanyamapori walao nyama (Simba, Chui, Duma).
Kabla ya maboresho ya miundombinu ya utalii TAWA ilikuwa inakusanya Tsh Millioni 1 Kwa Mwaka, lakini baada ya maboresho kiasi kisichopungua Tsh Millioni 50 Kwa Mwaka.