WANANCHI MILIONI 5.3 WANUFAIKA NA MIRADI YA MAJI
DAR ES SALAAM
Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2024, miradi 354 kati ya miradi 998 ya maji iliyopokea fedha kutoka Mfuko wa Taifa wa Maji imekamilishwa na hivyo kuwanufaisha wananchi takribani milioni 5.3 kwa huduma bora za maji.
Aidha serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji imeendelea kutekeleza miradi ya uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo takribani miradi 104 ya uhifadhi na uendelezaji wa vyanzo vya maji imetekelezwa.
ZINGATIA:- Serikali itaendelea kusimamia miundombinu ya maji ili kuzuia upotevu pamoja na wizi wa maji ili kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.