JAPAN KUONGEZA NGUVU  HUDUMA YA AFYA YA TZ

 

JAPAN KUONGEZA NGUVU  HUDUMA YA AFYA YA TZ

JAPAN KUONGEZA NGUVU  HUDUMA YA AFYA YA TZ

MWANZA
Serikali ya Japan imesisitiza dhamira yake ya kuongeza nguvu kwenye sekta ya afya ya Tanzania katika jitihada za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.(Hii ni kwa mujibu wa Balozi wa Japan nchini, Yashushi Misawa, wakati wa uzinduzi wa kliniki ya kisasa ya afya ya mama na mtoto katika hospitali ya Sumve wilayani Kwimba mkoani Mwanza).
Balozi Misawa amesisitiza kuwa uhusiano wa muda mrefu kati ya Japan na Tanzania umekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha mradi huo.
Katika ziara yao jijini Mwanza, ujumbe wa Balozi Misawa ulitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure, ambapo aliupongeza uongozi kwa kujitolea kwao katika kutoa huduma bora za afya.
Alisisitiza kuwa, pamoja na jitihada za Tanzania za kuboresha miundombinu ya afya, serikali ya Japan itaendelea kuunga mkono mipango ya serikali ya awamu ya sita inayolenga kuendeleza huduma za afya kwa wanawake na watoto.
"Serikali ya Japani imejitolea kusaidia Tanzania ili kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wanapata huduma bora za afya na kwamba maisha yao yanalindwa," amesema.