TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA MAFUNZO YA USAFIRI WA ANGA

 

TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA MAFUNZO YA USAFIRI WA ANGA

TANZANIA KUANZISHA KITUO CHA MAFUNZO YA USAFIRI WA ANGA

ARUSHA 
Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  inatarajia kutangaza zabuni ya ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga (CATC) kabla ya mwisho wa mwezi huu Novemba 2024. 
Makadirio ya gharama ya mradi wa CATC ni dola za Marekani milioni 34.6 (takriban shilingi bilioni 78.07  ikiwa na pamoja na VAT).
Hadi hivi sasa maandalizi yote yamekamilika na zabuni ya ujenzi wa kituo hicho itatolewa kabla ya mwisho wa Novemba na mradi huu unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka mitatu, kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 na kuhitimishwa 2025/26. 
Aidha Kituo hiki kitatoa mafunzo kwa wataalam katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa usafiri wa anga, usimamizi wa taarifa za anga, mawasiliano, ufuatiliaji, usalama wa anga, uendeshaji wa viwanja vya ndege, programu za mafunzo kwa wakufunzi na usimamizi wa anga.
ZINGATIA:- Mara baada ya kukamilika, kituo hicho kitakuwa kituo kikuu cha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.