TSH TRIL 6.7 ZALETA MAGEUZI SEKTA YA AFYA

 

TSH TRIL 6.7 ZALETA MAGEUZI SEKTA YA AFYA

TSH TRIL 6.7 ZALETA MAGEUZI SEKTA YA AFYA

TANZANIA
Kiasi cha shilingi trilioni 6.7 kilichotolewa ndani ya kipindi cha uongozi wa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kimesaidia mno kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya afya nchini  hasa upatikanaji wa huduma bora za afya ikiwemo matibabu ya kibingwa nchini.
Uwekezaji huu umeleta mabadiliko makubwa katika huduma za afya, hali ya ubora wa huduma za afya umeendelea kuimarika nchini na hospitali zote za rufaa sasa zimepata vifaa vya kisasa, ikiwemo CT Scan, huku hospitali za kanda zikifungwa mashine ya MRI, hatua inayomuweka Rais Samia katika rekodi za kihistoria.
Vilevile kutokana na maboresho ya sekta ya afya yamesaidia mno kupunguza vifo vya wajawazito kutoka 556 hadi 104 ambapo mafanikio hayo yanaonesha upunguzaji wa asilimia 81.2 katika vifo vya uzazi.