DKT SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE, KIFO CHA BONIFACE MPANGO (KING KIKII)

 

DKT SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE, KIFO CHA BONIFACE MPANGO (KING KIKII)

DKT SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE, KIFO CHA BONIFACE MPANGO (KING KIKII)

DAR ES SALAAM
Mhe Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan ametumia mitandao yake ya kijamii kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’
“Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’. 
Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania, na amekuwa mlezi na mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki. 
Tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema”
Amina.
BimkubwaTanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuwapa pole familia,ndugu,jamaa na watanzania wote kwa ujumla, Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.