TSH MIL 400 KUKABILIANA MABADILIKO YA TABIANCHI
TANGA
Serikali inatarajia kupeleka kiasi cha shilingi milioni 400 kwenye maeneo ya ukanda wa bahari ya Hindi Wilayani Mkinga Mkoani Tanga ili kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.
Wilaya ya Mkinga ni miongoni mwa wilaya ambazo zimeathiriwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hivyo Ili kunusuru hali hiyo uwepo wa mradi huo utaweza kumaliza changamoto hiyo lakini na kutoa fursa ya ajira ya Kudumu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi
Uwepo wa mradi huu unakwenda kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo tayari yameshaanza kuonekana katika maeneo ya bahari Kwa kingo za ardhi kuanza kutafunwa na bahari.
