TSH BIL 868.656 MIKATABA YA MIUNDOMBINU
TANZANIA
Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), imesaini mikataba 93 yenye thamani ya shilingi bilioni 868.656 ya ujenzi wa barabara za dharura na madaraja yaliyoharibiwa na mvua za El Niño na Kimbunga Hidaya katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha serikali kupitia TANROADS inaendelea na utekelezaji wa miradi 87 ya barabara zenye urefu wa kilometa 3,140.7 ikiwa ni pamoja na madaraja na viwanja vya ndege.
Asilimia 90 ya miradi iliyosainiwa itatekelezwa na wakandarasi wazawa kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt Samia kuwainua na kuwawezesha wakandarasi wazawa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.
ZINGATIA:- Mikataba 93 iliyosainiwa itatekelezwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Singida, Mikoa ya Songwe, Shinyanga, Tanga na Kigoma.