TANZANIA KUANZA UZALISHAJI WA NIOBIUM

 

TANZANIA KUANZA UZALISHAJI WA NIOBIUM

TANZANIA KUANZA UZALISHAJI WA NIOBIUM

TANZANIA
Tanzania inatarajia kuanza kuzalisha madini adimu ya niobium ambayo yanatumika katika tasnia mbalimbali ikiwemo ya kutengeneza ndege na injini za roketi.
Mradi wa uchimbaji wa madini ya niobium katika eneo la Panda Hill unamilikiwa na Kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited (PHTL), ambayo itazalisha bidhaa zinazotokana na niobium, ikiwamo ferronobium.
Aidha serikali imeanzisha majadiliano na Panda Hill ili kurasimisha makubaliano yatakayoiwezesha serikali kupata hisa katika mradi huo na kupata manufaa ya ziada ya kiuchumi.
Kuhusu hisa za Serikali katika mradi huo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura ya 123, wamiliki wa leseni za uchimbaji wa kati na wakubwa wanatakiwa kutenga angalau asilimia 16 ya hisa za riba kwa serikali. .
Pia  kikao cha kuhitimisha vipengele vya mkataba kimefanyika Novemba Mosi jijini Arusha ambavyo ni pamoja na jukumu la serikali katika uzalishaji wa niobium, ushiriki wake katika kituo cha usindikaji na uundaji wa kampuni tanzu kulingana na matakwa ya kisheria.
Baada ya mchakato wa kisheria kukamilika na zoezi la  utoaji wa leseni ya Ukanda wa Usindikaji wa Mauzo ya Nje (EPZ) kwa wawekezaji na serikali kuruhusu ujenzi wa haraka wa kiwanda hicho, kitakuwa cha kwanza cha aina yake nchini Tanzania na cha nne duniani.