TSH BIL 337.38 MATENGENEZO YA BARABARA KAGERA
KAGERA
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 337.38 kwa ajili ya matengenezo ya barabara mkoa wa Kagera ambapo hadi hivi sasa miradi kadhaa imeanza kutekelezwa kupitia bajeti hiyo katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Mkoa wa Kagera una mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 1,966.29 Kati ya hizo, kilometa 861.5 ni barabara kuu, kilometa 1,053 ni barabara za mikoa na kilomita 51.79 ni za wilaya, mijini na barabara kuu.