DKT SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA BW.MAFURU
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia, waziri wa nchi, Ofisi Ya Rais (Mipango na uwekezaji) kufuatia kifo cha Bw.Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea Novemba 9,2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Dkt Samia ameandika " Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema Amina"
Bimkubwatanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuipa pole na faraja familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.