TSH BIL 2.1 KUFIKISHA UMEME JUA BUKOBA, MULEBA  

 

TSH BIL 2.1 KUFIKISHA UMEME JUA BUKOBA, MULEBA

TSH BIL 2.1 KUFIKISHA UMEME JUA BUKOBA, MULEBA

KAGERA
Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) itatumia Sh bilioni 2.1 kufikisha umeme wa jua katika visiwa vya Ziwa Victoria vilivyopo Wilaya ya Bukoba na Muleba Mkoani Kagera ikiwa ni mpango maalumu wa kuwawezesha mwananchi kupata huduma hiyo.
Serikali imedhamiria kuhakikisha visiwa vyote ambavyo havijafikiwa na Gridi ya Umeme wa Taifa vinapata umeme kwa chanzo kinachoweza kutoa umeme huku gharama ya asilimia 55 hadi 75 ikibebwa na serikali kulingana na ukubwa wa huduma inayotolewa kwa wananchi na wafanyabiashara walioko visiwani.
Aidha katika umeme ambao umefungwa katika kisiwa Cha Musira kaya 192 zinatarajia kunufaika huku kaya 50 tayari zimeishaanza kutumia mfumo huo,na maeneo yanayotoa huduma za umma kama shule ,Makanisa,misikiti tayari nao wameanza kutumia mfumo huo.
FAHAMU:- Mikoa 7 ya Tanzania, wilaya 16 na kata 43 pamoja na visiwa 118 nchini vitanufaika na umeme jua kwa gharama ya Sh bilioni 8.