![]() |
MHE.RAIS DKT SAMIA ATOA POLE, KUPOROMOKA GHOROFA KARIAKOO
TANZANIA
Kufuatilia ajali ya kuporomoka ghorofa iliyotokea leo Novemba 16, 2024 kariakoo Jijini Dar es Salaam Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa waathirika wa ajali hiyo.
Kupitia mitandao ya kijamii Dkt Samia ameandika.
"Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.
Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii"
Bimkubwatanzania tunaungana na Mhe Rais Samia kuwapa Pole wote waliopatwa na kadhia hii
"Pole sana kariakoo, hili nalo litapita".