TSH BIL 143 ZAONGEZA MAJI SIKONGE, KALIUA
TABORA
Kiasi cha shilingi bilioni 143 kinatekeleza Mradi wa maji wa miji 28 ikiwemo sikonge,Urambo na kaliua Mkoani Tabora inayotekelezwa na mkandarasi Megha Engineering ambayo imefikia asilimia 50 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2025.
Kukamilika kwa miradi hiyo ya maji katika maeneo hayo kutafanya upatikanaji wa maji kwa Sikonge, Urambo na Kaliua kuwa zaidi ya asilimia 90 na wakazi 490,000 watapata huduma ya majisafi na salama.
