DKT SAMIA KUANZA ZIARA HAVANA,CUBA
TANZANIA
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili Havana, Cuba ( leo) Novemba 6 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, inayotarajiwa kwa kiasi kikubwa kufungua fursa za kijamii na kiuchumi na kuimarisha uhusiano wa kihistoria wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Akiwa nchini Cuba, Mhe Rais Dkt Samia anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Miguel DÃaz-Canel Bermudez Novemba 7, anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili mjini Havana, nchini Cuba kuanzia Novemba 7 hadi 10, 2024
Dkt Samia atapata fursa ya kuweka shada la maua kwenye Kumbukumbu ya José MartÃ, ikiwa ni ishara ya kumuenzi shujaa wa taifa la Cuba na kuzindua sanamu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika eneo maalum la Mashujaa wa Afrika mjini Havana.
Ziara hiyo pamoja na masuala mengine, itajikita zaidi katika ushirikiano wa pande mbili na changamoto za kimataifa zinazohitaji masuluhisho ya pamoja kwa manufaa ya pande zote.
Pia, inalenga kuziwezesha Tanzania na Cuba kuendeleza uhusiano wao wa kihistoria na kidiplomasia kwa kufungua njia mpya za ushirikiano wenye maslahi ya kiuchumi na kijamii.
Tupo tayari kukuhabarisha @bimkubwatanzania