MIRADI 63+ KUPANUA BIASHARA YA KABONI

 

MIRADI 63+ KUPANUA BIASHARA YA KABONI

MIRADI 63+ KUPANUA BIASHARA YA KABONI

TANZANIA
Tanzania imesajili  zaidi ya miradi 63 ya biashara ya kaboni katika sekta mbalimbali na kuiwezesha nchi kupunguza kasi ya hewa ukaa na kuingiza mapato kutokana na huduma za mazingira. 
Miradi iliyosajiliwa ni sekta ya kilimo (asilimia 8), nishati (asilimia 33), misitu (asilimia 51), mifugo (asilimia 5) na udhibiti wa taka (asilimia 3).
Kati ya miradi iliyosajiliwa chini ya sekta ya misitu,  inahusisha upandaji miti,  huku ikilenga kupunguza uharibifu na upotevu wa misitu, na kurejesha uoto wa asili
Aidha, Serikali inatekeleza Mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia (2024-2034), unaohimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kama vile gesi asilia, nishati mbadala, mkaa mbadala na umeme ambapo mpango unahimiza hadi kufikia mwaka 2034 zaidi ya 80% ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.