HIZI HAPA HOSPITALI  ZA UTALII TIBA

 

HIZI HAPA HOSPITALI  ZA UTALII TIBA

HIZI HAPA HOSPITALI  ZA UTALII TIBA

TANZANIA
Tanzania imechagua hospitali ili kuendesha mpango wa utalii wa kimatibabu (Utalii tiba) ambazo ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Aidha uwekezaji katika utalii wa matibabu ni endelevu na hospitali za rufaa zitajengwa katika kanda zote nchini na  mipango iko tayari kuwa na kituo kingine kikubwa cha rufaa mkoani Kigoma kitakachotoa huduma za matibabu ikiwemo utalii wa matibabu.
Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu ya matibabu, kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya katika ngazi za madaktari bingwa.