DKT SAMIA AONGEZA CHACHU MATUMIZI YA KISWAHILI MAHAKAMANI

DKT SAMIA AONGEZA CHACHU MATUMIZI YA KISWAHILI MAHAKAMANI

DKT SAMIA AONGEZA CHACHU MATUMIZI YA KISWAHILI MAHAKAMANI

TANZANIA
Katika kuimarisha utoaji wa haki nchini, Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan  imeendelea kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kutoa huduma za kimahakama pamoja na uandishi wa nyaraka za kisheria.
Ili kuongeza ufanisi zaidi kwenye kuimarisha utolewaji wa haki nchini mwaka 2024, umeandaliwa Mwongozo wa Mahakama wa kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika uendeshaji wa kesi na uandishi wa hukumu,  sheria kuu 258 na sheria ndogo 15,000 zimetafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili