DKT SAMIA AELEKEA BRAZIL KUSHIRIKI MKUTANO G20
DAR ES SALAAM
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo Novemba 16, 2024 kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa kundi la G20.
Mhe.Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Ińacio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.
#BimkubwaG20