JENGO LA WAHISIWA MAGOJWA YA MLIPUKO LAKAMILIKA
KAGERA
Serikali imekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la kuwahifadhi wahisiwa wa magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza lililopo katika mpaka wa Mutukula wilaya ya Missenyi mkoa wa Kagera, ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 140 ambalo limewekewa huduma za maji, umeme na vitanda na tayari limeanza kutumika.
Aidha kwa mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 80 kwa ajili ya maboresho ya sehemu ya nje ya jengo, ikiwemo kuweka sehemu yenye kivuli kwa ajili ya wasafiri pamoja na uwekaji wa viyoyozi na samani nyingine kwa ajili ya utoaji wa huduma.
MUHIMU:- Lengo la Serikali ni kuhakikisha magonjwa ya mlipuko hayaingii nchini ndio maana inaweka miundombinu bora na kujikinga katika maeneo yote ya mipakani.