TSH TRIL 4.6 ZINAJENGA BARABARA, MADARAJA

 

TSH TRIL 4.6 ZINAJENGA BARABARA, MADARAJA

TSH TRIL 4.6 ZINAJENGA BARABARA, MADARAJA

TANZANIA
Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) yenye thamani ya Sh trilioni 4.6.
Kupitia miradi hiyo tayari Tanroads imekamilisha kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Sh. trilioni 1.68 katika kipindi cha utawala wa Mhe. Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan.
Pia hadi sasa Sh bilioni 101.1 zimelipwa kwa wakandarasi katika miradi 24 ya ujenzi wa barabara inayoendelea kutekelezwa pamoja na miradi ya minne (4) ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini
Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inaendelea kwa kasi maeneo mbalimbali nchini na hakuna mradi uliokwama kwasababu Serikali imekuwa ikilipa wakandarasi kulingana na mikataba.
MUHIMU ZAIDI:-  Tangu Dkt Samia aingie madarakani ameweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kurahisisha usafiri na usafirishaji lengo likiwa ni kukuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja