ZAHANATI KUHUDUMIA WANANCHI 2,000 MAPARAWE

 

ZAHANATI KUHUDUMIA WANANCHI 2,000 MAPARAWE

ZAHANATI KUHUDUMIA WANANCHI 2,000 MAPARAWE

MTWARA
Zaidi ya wakazi 2,000 wa kijiji cha Maparawe kata ya Mchauru wilayani Masasi mkoani Mtwara wananufaika na mradi wa ujenzi wa zahanati uliogharimu zaidi ya Shilingi milioni 75.
Kabla ya mradi huu wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakitembea umbali mrefu wa takribani kilometa 10 kwenda vijiji jirani kufuata huduma hiyo.
Mkazi wa kijiji hicho, Haruna Awadhi amesema:  “Tumefurahi sasa mama Samia kutuletea mradi huu wa zahanati kwasababu umeturahisishia kwenda vijiji jirani kufata huduma ya zahanati, tulikuwa tunateseka sana tulikuwa tunaenda vijiji jirani kama vile sindano na hadi kufikia hatua hii tunashukuru sana.”
Aidha zahanati hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo ya akina mama wajawazito, wagonjwa wa nje na zingine.