UKARABATI, UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE TABORA SASA NI 72%

 

UKARABATI, UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE TABORA SASA NI 72%

UKARABATI, UPANUZI KIWANJA CHA NDEGE TABORA SASA NI 72%

TABORA
Ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora umefikia asilimia 72 huku  jengo la abiria likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria 120 kwa wakati mmoja litakapokamilika.
Mradi huu pia unahusisha barabara ya kuruka na kutua ndege, mnara wa kuongozea ndege, barabara za maingilio na maegesho ya ndege na barabara ya kuingia katika kiwanja cha ndege, maegesho ya magari, uzio wa usalama na kituo cha hali ya hewa"
Ujenzi wa kiwanja hicho unatekelezwa na mkandarasi Beijing Construction Engineering Group Co, kutoka China kwa gharama ya shilingi bilioni 24.6.
Kiwanja cha ndege cha Tabora kilianzishwa mwaka 1940 na kimekuwa kikiboreshwa mara kwa mara na kukamilika kwake kutawezesha ndege nyingi kubwa kukitumia kiwanja hicho na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi katika Mkoa wa Tabora na ukanda wa magharibi kwa ujumla.