WANAFUNZI 252,000 KUNUFAIKA NA MIKOPO HESLB
TANZANIA
Serikali kupitia bodi ya mikopo (HESLB) inatarajia kutoa mikopo kwa jumla ya wanafunzi 252,000, wakiwemo wanafunzi 80,000 wa mwaka wa kwanza ambapo jumla ya shilingi bilioni 787 zimetengwa.
Aidha Katika mwaka uliopita, wanafunzi 79,200 wa mwaka wa kwanza walipata mikopo, na kuvuka lengo la 75,000, huku wanafunzi 146,000 wanaoendelea nao wakinufaika na mikopo ya elimu ya juu.
