TSH BIL 3.6 ZA SAMIA SCHOLARSHIP KUWANUFAISHA WANAFUNZI 700

 

TSH BIL 3.6  ZA SAMIA SCHOLARSHIP  KUWANUFAISHA  WANAFUNZI 700

TSH BIL 3.6  ZA SAMIA SCHOLARSHIP  KUWANUFAISHA  WANAFUNZI 700

ARUSHA
Kiasi cha shilingi bilioni 3.6  kimetengwa kwa ajili ya kuwanufaisha wanafunzi wapatao 700 wa elimu ya juu nchini wanaosoma chini ya  mpango wa ufadhili wa  Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  (SAMIA SCHOLARSHIP) kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025 ( Hii ni kwa mujibu wa Ufunguzi wa kikao kazi cha 13 cha siku mbili cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kilichowakutanisha maofisa mikopo na wawakilishi wa wanafunzi jijini Arusha)
Pamoja na kuongeza ufadhili wa mikopo ya elimu ya juu, mpango wa ufadhili wa masomo unaolenga zaidi masomo ya sayansi, unalenga pia kukuza kizazi kipya cha wataalam katika fani hiyo muhimu.
Aidha Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia imepanua utoaji wake wa ufadhili wa masomo na kuwajumuisha wanafunzi wa stashahada, kwa kutenga shilingi bilioni 24.8 kusaidia watu 7,000.
Kwa ujumla, Serikali imetenga Sh bilioni 787 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu kupitia HESLB kwa mwaka huu wa masomo.