WAKULIMA WAUZA KOROSHO TSH 4000+ @KG

 

WAKULIMA WAUZA KOROSHO TSH 4000+ @KG

WAKULIMA WAUZA KOROSHO TSH 4000+ @KG

MTWARA
Wakulima wa korosho  wanaouza korosho zao kupitia chama kikuu cha ushirika cha mazao cha TANECU Mkoani Mtwara leo Oktoba 11, 2024  wameandika  Historia baada ya kuuza korosho zao kwa bei ya juu Shilingi 4,120 na bei ya Chini 4,035 katika mnada wa kwanza wa msimu wa Korosho msimu 2024/2025 uliofanyika katika Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.
Mnada huo umefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Newala huku jumla ya tani 3,857 za Korosho kutoka TANECU zikipelekwa ghalani na zote  zimenunuliwa.
Msimu wa Korosho 2024/2025 umeanza wakati ambapo wakulima wana imani ya kuimarika kwa bei katika soko, huku uzalishaji ukitarajiwa kupanda kutokana na juhudi ambazo zimefanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kusimamia sekta ya Korosho nchini kama vile kutoa bure pembejeo za ruzuku kwa wakulima.