BANDARI YA TANGA YAVUKA LENGO UTOAJI HUDUMA
TANGA
Bandari ya Tanga katika kipindi cha Robo Mwaka ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2024/ 2025 imevuka malengo ya kuhudumia meli, shehena na mapato kuanzia Julai hadi Septemba 2024.
Katika kipindi cha Julai - Septemba, 2024 ilipangiwa kuhudumia meli 54 zenye uzito wa tani 444,249 lakini imehudumia meli 113 zenye uzito wa tani 627,091 ikiwa imevuka malengo kwa 109.3% na kipindi kama hicho cha Julai - Septemba 2023 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 bandari ilihudumia meli 44 zenye uzito wa tani 356,553.
Kipindi cha Julai - Septemba 2024 bandari iliwekewa malengo ya kuhudumia shehena ya mzigo tani 283,225 lakini ikaweza kuhudumia tani 333,643 sawa na ongezeko la asilimia 17.8. Pia Meneja amesema ukilinganisha na kipindi kama hicho Julai - Septemba 2023 kwa mwaka wa fedha uliopita wa fedha 2023/2024 bandari ilhudumia tani 204,290. Kwa hiyo ukilinganisha na mwaka huu kuna ongezeko la shehena kwa asilimia 63.3.
Aidha kwa upande wa mapato Bandari ya Tanga imefanya vizuri katika kukusanya mapato kwani kipindi cha Julai - Septemba 2024 ambapo ilipangiwa kukusanya Shilingi bilioni 11.393 lakini imeweza kukusanya Shilingi bilioni 18.631 ikiwa imevuka malengo kwa 63.5% kwa kulinganisha kipindi kama hicho Julai - Septemba 2023 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo ilikusanya Shilingi bilioni 11.127 wakati Julai - Septemba 2024 imekusanya Shilingi bilioni 18.631 Sawa na ongezeko la asilimia 130.05.
