UPANUZI CHUJIO LA MAJI MJINI GEITA 95%
GEITA
Serikali kupitia mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa chujio la maji Nyankanga mjini Geita na umefikia 95% ya utekelezaji.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika Octoba 30 na unatekelezwa kwa mikataba miwili yenye jumla ya Sh bilioni 1.17, na Mradi huu wa upanuzi wa chujio utaweza kuzalisha lita milioni 3 kwa siku na hivyo kuongeza uzalishaji wa majisafi kutoka lita milioni 4 kwa siku zinazozalishwa sasa mpaka lita milioni 7 kwa siku.
