TSH MIL 500 ZAWAJENGEA SHULE NANDA,NEWALA
MTWARA
Wakazi wa kjiji cha Nanda kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara wananufaika na mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Nanda uliogharimu Sh milioni 500.
Faida wanazozipata wakazi hao katika ujenzi wa mradi huo, ni pamoja na kuwaondolea adha wanafunzi kufuata elimu vijiji jirani.
Mradi huo hauwanufaishi wakazi wa Nanda pekee pia na wakazi wa vijiji vingine vya Mmovo, Mnali, Namkonda.
Baadhi ya wazazi kijijini hapo, akiwemo Hassan Halidi amesema “Tunaishukuru sana serikali yetu ya awamu ya sita kutujengea hii shule na kutuondolea adha ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule”
Vilevile baadhi ya wanafunzi shuleni hapo akiwemo Shadraki Ayubu kutoka kidato cha kwanza ameishukuru serikali kuwapelekea ujenzi wa shule hiyo kwenye kijiji chao kwa sababu umewarahisishia upatikanaji wa elimu.
