TSH TRIL 1 ZA BOT KUNUNUA DHAHABU

 

TSH TRIL 1 ZA BOT  KUNUNUA DHAHABU

TSH TRIL 1 ZA BOT  KUNUNUA DHAHABU 

GEITA 
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetenga shilingi trilioni 1  kwa ajili ya mpango wa ununuzi wa dhahabu wa ndani unaolenga kukuza hifadhi ya dhahabu nchini.
Mpango huo umeundwa ili kukabiliana na uhaba wa fedha za kigeni ambao umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za madini.
" BOT imetenga sh trillion 1 kwa ajili ya ununuzi, na malipo yanafanyika ndani ya saa 24, kuhakikisha tuko tayari kununua dhahabu," Rais Samia amesema wakati akifunga Maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita Oktoba 13, 2024.
Dkt Samia amesisitiza kuwa utekelezaji wa programu hii tayari unaendelea, ambapo marekebisho ya Sheria ya Madini chini ya Kifungu cha 59 yamefanyika, yakiwataka wamiliki wa leseni na wafanyabiashara wa madini kuuza asilimia 20 ya dhahabu wanayozalisha kwa BOT.
Aidha Mhe Rais Samia amesema kuwa benki kuu inatoa motisha ya kuvutia chini ya mpango huo ikiwemo kupunguza ada za mrabaha kutoka asilimia 6 hadi 4, kuondoa ada za ukaguzi, na kutoa VAT isiyokadiriwa, kuruhusu wauzaji kudai ushuru wa pembejeo.