TANZANIA, FINLAND KUIMARISHA UHUSIANO
FINLAND
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imefanya mazungumzo na Rais wa Finland Alexander Stubb mjini Helsinki nchini Finland kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili huku mazungumzo hayo yakisisitiza umuhimu wa uhusiano thabiti wa kidiplomasia ulioanzishwa katika miaka ya 1960.
Pamoja na mazungumzo hayo wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutana na Watendaji Wakuu mbalimbali wa makampuni makubwa yaliyochaguliwa nchini Finland ili kuhamasisha na kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania kwa wawekezaji watarajiwa.
