TSH BIL 20- KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 105 IRINGA

 

TSH BIL 20- KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 105 IRINGA

TSH BIL 20- KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 105 IRINGA

IRINGA 
Zaidi ya Shilingi bilioni 20 zitatumika kusambaza umeme kwenye vitongoji 105 katika majimbo ya Mkoa Iringa kupitia mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji awamu ya pili (HEP II) unaotekelezwa kwa miaka miwili kati ya sasa na Septemba 2026.
Kupelekwa umeme katika vitongoji hivyo kutafanya jumla ya vitongoji vyenye umeme kufikia 1,293 kati ya vitongoji 1,853 vya mkoa huo.
Mradi huo utakapokamilika utaziunganisha kaya za vitongoji hivyo na umeme, na unatazamiwa kuboresha maisha ya watu kwa kuongeza upatikanaji wa nishati, kuboresha huduma za afya, elimu, na fursa za kiuchumi.