TSH BIL 2.8 KUBORESHA AFYA , BIMA YA AFYA KWA WOTE IKIWEMO
DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wakala wa Maendeleo wa Umoja wa Afrika (AUDA NEPAD) wamesaini makubaliano ya ushirikiano yenye thamani ya dola milioni 1 takribani shilingi bilioni 2.8 zitakazotumika kwenye maeneo matano ya afya ikiwa ni pamoja na Bima ya Afya kwa wote na kuboresha afya ya uzazi.
Ushirikiano huo pia utawezesha kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawili kwa kila mitaa, ambao watasaidia kupambana na magonjwa ya milipuko na kupima magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Eneo lingine ni la afya ya uzazi kwa vijana waliopo shule za sekondari ambapo wamepanga kusaidia ili kuepuka mimba zisizotarajiwa kwa vijana hao na kuboresha vituo vya afya ya uzazi, ili kuokoa maisha ya watoto wachanga.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji MKuu wa AUDA NEPAD Bi. Nardos Bekele amesema,
"Tunayo furaha tuko hapa kushirikiana nanyi tunaunga mkono mnachofanya, hii itawezesha kukuza uchumi wa Afrika, hivyo kwa pamoja tunahakikisha kuwa jitihada zinazofanywa zinaungwa mkono na kuzaa matunda," amesema Bi. Bekele
Aidha Bi. Bekele ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo mengi mazuri anayoyafanya chini ya uongozi wake.
