RAIS SAMIA AMPONGEZA DANIEL CHAPO KUCHAGULIWA RAIS WA MSUMBIJI

 

RAIS SAMIA AMPONGEZA DANIEL CHAPO KUCHAGULIWA  RAIS WA MSUMBIJI

RAIS SAMIA AMPONGEZA DANIEL CHAPO KUCHAGULIWA  RAIS WA MSUMBIJI

TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan  kwa niaba ya serikali na wananchi wa Tanzania ametuma salamu za pongezi kwa Mhe Daniel Francisco Chapo (FRELIMO) kwa kuibuka mshindi katika kiti cha Urais kutokana na uchaguzi mkuu  uliofanyika Oktoba 9, 2024 nchini Msumbiji na baadae Oktoba 24  kutangazwa  mshindi na Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE) kwa kupata kura asilimia 70.67 ya kura zote.
Dkt Samia ametuma salamu hizo za pongezi kupitia mitandao ya kijamii ambapo ameandika
“On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency, Daniel Francisco Chapo, President-elect of the Republic of Mozambique, on your victory in the 2024 Mozambican General Election. I am looking forward to working together in fostering the historic, economic and diplomatic relations between Tanzania and Mozambique”
“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Mhe. Daniel Francisco Chapo, Rais Mteule wa Jamhuri ya Msumbiji, kwa ushindi wako katika Uchaguzi Mkuu wa 2024 wa Msumbiji. Natarajia kufanya kazi pamoja katika kukuza uhusiano wa kihistoria, kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na Msumbiji”
BimkubwaTanzania tunaungana na Mhe.Rais Dkt Samia kukutakia kila la kheri katika majukumu yako Mhe Daniel Francisco Chapo.