TSH BIL 42.24 KWENYE TSMP II

 

TSH BIL  42.24 KWENYE TSMP II

TSH BIL  42.24 KWENYE TSMP II

TANZANIA
Benki ya Dunia (WB) imetangaza  kwamba itatenga shilingi  bilioni 42.24  kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Takwimu Tanzania Awamu ya Pili (TSMP II).
Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bw. Dhiraj Sharma taarifa hii  wakati wa mkutano na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa mpango huo.
Bw. Dhiraj amesema  kuwa benki iliweka vigezo kumi na tatu vya tathmini, ambapo kumi na moja vilifikiwa, na hivyo kuidhinisha awamu ya ziada ya ufadhili wa dola za Marekani milioni 15.5 (takriban  shilingi bilioni 42.24).
“Kwa Benki ya Dunia kutoa ufadhili wa mradi huu, tulitaka kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika awamu iliyopita. Tumeridhishwa na matokeo,” Bw Sharma amesema.
Serikali, chini ya uratibu wa NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS), inatekeleza TSMP II, ambayo inatoa mfumo madhubuti wa maendeleo ya takwimu rasmi nchini.
Mpango huu wa miaka mitano, unaojumuisha kipindi cha kuanzia 2022 hadi 2027, unatekelezwa bara na visiwani kwa mkopo wa riba nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 82 kutoka Benki ya Dunia.