TSH BIL 100 KUPELEKA-UMEME-VIJIJINI
KIGOMA
Serikali kupitia wakala wa Nishati Vijijini (REA) itatumia zaidi ya Sh Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma unaolenga kuboresha shughuli za kiuchumi za wananchi wa vijijini mkoani humo.
Katika mkoa wa Kigoma jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na huku Katika vitongoji 1849 vilivyopo Mkoa wa Kigoma vitongoji 1370 tayari vimeshapata umeme.