DKT SAMIA ATOA POLE, AAGIZA UMAKINI BARABARANI
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa pole kufuatia ajali za barabarani zilizotokea katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro na kusababisha vifo na majeruhi
Kupitia mitandao ya kijamii Dkt Samia ameandika.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali za barabarani zilizotokea katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro na kusababisha vifo na majeruhi. Nawapa pole wafiwa wote, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawaombea marehemu wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka”
Pia Mhe. Samia ametoa wito kwa watumiaji wa barabara kuongeza umakini ili kuepusha ajali za barabarani
“Tunapoelekea mwishoni mwa mwaka, nawasihi watumiaji wote wa barabara kuongeza umakini”
Aidha Dkt Samia ameandika “Nimeziagiza mamlaka zote husika kuongeza umakini katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani. Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina”
BimkubwaTanzania tunaungana na Mhe.Rais Dkt Samia kuwapa pole Watanzania wote walioguswa na vifo hivi na Mwenyezi Mungu awape nguvu familia zao katika kipindi hiki kigumu.
