TSH BIL17.9 KUPELEKA UMEME  KAYA 5,478. MOROGORO

 

TSH BIL17.9 KUPELEKA UMEME  KAYA 5,478. MOROGORO

TSH BIL 17.9 KUPELEKA UMEME  KAYA 5,478 MOROGORO

MOROGORO
Serikali kupitia  Wakala wa Nishati Vijijini (REA)  imesaini mkataba na kampuni ya SINOTEC CO. LTD kwa ajili ya kutekeleza mradi wa umeme wenye thamani ya sh bilioni 17.9 unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 24 na utakapokamilika utanufaisha zaidi ya kaya 5,478.
 Kati ya vijiji 669 katika Mkoa wa Morogoro, vijiji 652 ambavyo ni sawa na asilimia 97.5 vimefikiwa na nishati ya umeme na vijiji 17 vilivyobaki viko kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji ili navyo vipate umeme.
 Aidha Mkoa wa Morogoro una vitongoji 3,369 na katika hivyo, vitongoji 1,655 sawa na asilimia 49 tayari vimepatiwa umeme.